Tuesday, November 26, 2013

 Fashion Mustafa.  Ni website ambayo imetengenezwa na Shekha Khamisi akiwa kama mteja wake ambaye alikuwa anahitaji website katika kutangaza bidhaa zake ambapo mteja wake anahusika zaidi na mtindo akiwa anauza nguo mbalimbali zinazohusiana na mitindo na fasheni kiujumla kama tunavyoijua fasheni ilivyo. Katika maisha kama vijana , wazee na watoto kama hujazingatia fasheni utaonekana kituko ndani ya jamii kwa ndio maana suala la fasheni ni la muhimu sana kuzingatiwa ili kuweza kuendana na wakati uliopo. Mstafa fashion ameamua kuwasogezea wateja wake huduma kwa karibu zaidi ili wasisumbuke kwenda hadi nchi za wengine kutafuta mahitaji kama hayo tena kwa bei ambayo hata mimi mwenyewe nilishindwa kuamini kama kweli bidhaa bora kama zile zinaweza kupatikana kwa bei nafuu kama ile. daaah!!!! kajionee mwenyewe.
 Hi hapa ni ukurasa wa ndani unaoonesha zaidi mitindo mbalimbali anayouzika sehemu hizo.
 Jipemoyo Center. Kituo kinachohusika na uleaji wa watoto walio katika sehemu mbalimbali, ambapo wanachukua watoto kutoka sehemu mbalimbali wakiwa  makao yao makuu musoma. hii ni website ambayo imetengeneza na kijana kutoka katioka Chuo chetu cha Musoma Information Center. aitwaye Baraka Richard.
 Huu hapa ni ukurasa wa ndani wa website hiyo ambayo imetengenezwa na kijana huyu ambaye nae ametokea katika kituo hichohicho na kujiunga nasi na akawa amepata ujuzi huo juu ya kutengeneza tovuti huyo.
 Annastella Gervase. Ni mwanachuo kutoka katika chuo cha Musoma Information Center ambaye anahusika na web design and developing akiwa amepewa kandarasi hii ya kuwatengezea Givalen Motel Limit website ambayo itasaidia kuwatangaza kimataifa kulingana na huduma wanazozitoa huko. kiukweli ni moja kati ya hotel nzuri kabisa yenye hadhi ya kimataifa ikiwa inapatikana mkoani mara wilaya ya musoma. kiukweli kutokana na huduma zao kuwa bora ndio maana msichana huyu alichukua muda na akakaa chini kufiria ni jinsi gani anaweza watengenezea tovuti yenye kiwango cha kimataifa na kama unavyoiona hapo juu inakiwango cha kimataifa na kiukweli hakuwangusha juu ya hilo.
 Huu hapa ni ukurasa wa ndani ya tovuti hiyo, ukielezea zaidi kuwahusu hao givalen motel na vitu vingi kuwahusu wao.
 Community alive. Tasisi inayohusika na utunzaji au uleaji wa watoto ambao hawakuweza kupata nafasi ya kupata mahitaji muhimu kutoka kwa wazazi wao kutokana na matatizo mbalimbali kama :- UKIMWI, mfarakano wa wazazi hadi kupelekea kutengana, maisha magumu katika familia mambayo yanasababishwa na wazazi kutokuwa na elimu juu ya kujipanga na kuweka akiba kwa ajili ya watoto wao watakaozaliwa hivyo basi wanafikia wakati wanapata watoto na huku hawanachochote. wameamua kutengeneza website ambayo itawatangaza kitaifa na kimataifa pia ili waweze kupata wafadhili pia kupanua wigo wa kuwasaidia watoto hao. hivyo basi hii hapa ni tovuti walitengenezewa na Mmoja kati ya wanachuo cha musoma Information Center aitwaye Janepha Nassoro.
Karibu sana Community Alive.

 Moja kati ya sehemu ambayo wewe kama mzee, bibi , Kijana, Mtoto unaweza kukaa ukafurahia siku yako kutokana na mafanikio uliyoyapata au unataka kuondoa msongo wa mawazo yanayokusumbua au unahitaji maombezi kutoka kwa mapadri ambao kiukweli wamebarikiwa kwa neno la mungu si pengine ni EPHETA. Hii hapa ni sehemu maalumu ikiwa na uwanja mkubwa kabisa ambao umezungukwa na beach ambapo unaweza ukaingia na ukafurahia siku yako kiukweli mi ni mmoja wao wa ambao walishawahi kufika sehemu hii ndio maana nakupasha haya machache. sehemu hii inapatikana Makoko wilayani musoma Mara. Karibu sana.
ukumbi wa maombezi kwa wanaomhitaji mwenyezi mungu . Tovuti hii ikiwa inaandaliwa na mmoja kati ya wanachuo wetu wa Musoma Information Center Esagara Meru

 Ujue Mkoa wa Mara kupitia tovuti Hii ya (History of Mara Region and Its District)
sehemu pekee ambapo unaweza gundua mengi kuuhusu mkoa wa mara na matukio yake ambayo kila siku unayaona kwenye runinga mengine yakiwa ni ya kweli mengie ni yale wanayo yatunga wandishi wa habari ili mkono upate kwenda kinywani. kiukweli utaweza kujua historia ya mkoa wa mara na makabira yake makuu, vyakula wanavyopendelea kuvitumia, Biashara zao, tamaduni zao na mengineyo mengi. usikose kupata link ya website hii pindi itakapokuwa imekamilika hapa hapa katika blog hii, hii tovuti bado iko jikoni ikipikwa na mwanachuo wetu ajulikanae kama Sarah Linkolini Usikose uhondo huu.
ukurasa wa ndani ambao sasa utakuwa unapata nafasi ya kusoma habari zenyewe kwa undani zaidi

Bakhita English Medium Primary School, ni shule ambayo inahusika na utoaji wa elimu ya pre-primary na primary school kwa watoto wadogo. shule hii inafundisha kwa lugha ya kiingereza. shule hii inajitahidi sana na imekuwa ikishika nafasi za juu kimkoa na kitaifa pia na imejikusanyia umarufu kwa njia hiyo ni shule ya kidini ambayo watoto wanalelewa kwa maadili ya kidini kuanzia mwanzo wanapokuwa wamejiunga na shule hadi wanapokuwa wanahitmiu hivyo basi kutokana na suala la maadili kiukweli vijana unakuta wameiva. wamefikia wakati wakaona ni bora wawe na tovuti yao ya kuwatangaza wao pia na kutangaza shule yao kiujumla, hawakusita kutuamini kutokana na kazi tunazozifanya hivyo basi wakawa wamempa kijana wetu kandarasi hiyo ambaye anaenda kwa jina la Rosi Ladislausi
Baraki sister Farm. kiukweli sijui nikueleze nini juu ya huu mradi kiukweli mimi mwenyewe natafuta jina ambalo linaweza kuwa mbadala wa mradi huu lakini linaniwia vigumu kulipata na hii ni kutokana na niliyoyaona hapo kwa macho yangu mwenyewe bila kusimuliwa na mtu, kiukweli huwezi kuamini kuwa mradi huu unaendeshwa na mwanamke , ama kweli wanawake wakiamua wanaweza hilo ndilo lilikuwa jibu langu nilipofika eneo hilo. Huu mradi unaendeshwa na mwanamke ambaye amejitolea maisha yake yote kwa mwenyezi mungu ambao sisi tunawaita ( Masisiter ). akiwa anaendesha mradi huu mkubwa wenye miradi mingine tena mikubwa ndani yake. Baadhi ya miradi ambayo mi mwenyewe niliiona kwa macho yangu ni mradi wa samaki ambapo wana Dimbwi kubwa lenye maji ya kutosha na samaki wa kutosha kabisa  lenye umbali wa Km 90 za Mraba, mradi wa ng'ombe wa kisasa wa maziwa wakiwa kila siku wanapata Lita za maziwa zisizopungua 200, Mradi wa ufugaji kuku wa nyama na mayayi wa kisasa kabisa niliona kuku wa kutosha kabisa japo sikuweza kuwahesabu lakini kwa makadilio ni kama kuku 3000.
kiukweli kijana huyu anayejaribu kutengeneza tovuti hii bado ana kazi ya ziada kuweza kuhakikisha kuwa vitu vyote hivyo vinaonekana kwenye tovuti yao ili wateja watakao tembelea tovuti hii wapate kujua vitu vyote hivyo vinavyofanyika huko. Kijana huyu si mwingine bali ni Victor Mwita Mandara kutoka Musoma Information Center.
Kigera Saccos. Ni saccos kama tunavyojua kwamba wanahusika na utowaji wa mkopo kwa watu mbalimbali wenye vipato tofauti tofauti wa kipato cha chini wenye vipato vya juu. kupitia saccos unaweza ukapata mkopo pia unaweza ukatunza pesa zako kwa usalama zaidi. hivyo basi wameona ni vema wakawa na website kwenye mtandao ambayo itawasaidia kutangaza huduma zaidi kwa ufanisi wa hali ya juu kitaifa na kimataifa. hivyo basi walichukuwa nafasi hii na kumjaribu kijana wetu wa kike kuwa ameiva kiasi gani katika mambo haya ya design, hakika binti huyu nae alipopata nafasi hii aliamua kuwaonesha kuwa tayari ameishakuwa kuwa mtaalam katika mambo haya na akawa amewatengenezea tovuti ambayo hata wao hawauweza kumini kama wangeweza kuopata tovuti yenye ubora wa kiwango cha kimataifa kama zilivyo huduma zao si mwingine aliyetengeneza tovuti hii bali ni Elizabeth Joseph wa Musoma Information Center

0 comments:

Post a Comment