"Hot flower " Hapa ni lugha ya kigeni ambayo imetumika hapo lakini hapa utapata nafasi ya kuelezewa juu ya Madawa ya kulevya hasahasa ( jani a.k.a BANGI ) Mhusika ameamua kupunguza ukali wa maneno lakini anayo elimu ya kutosha kichwani ambayo angependa kukushirikisha katika kutambua matatizo haya ya uvutaji wa bangi na madhara yake. karibu tumsikilize pale ambapo atakuwa tayari ameweka tayari maelezo yake kupitia website yake.
Deigned by Mark |
Designed By Annastella Gervas |
Wewe amabaye unasumbuliwa na Matatizo ya kukasirika mara kwa mara kumbe unaweza ukawa umepata dawa ya moja kwa moja na bila kutumia gharama kubwa maana wengi wetu wameenda kwa waganga kwa kutafuta madawa kwa gharama kubwa. Sasa unaweza ukawa umepata dawa kupitia elimu ya huyu mwanadada. karibu kwa msaada zaidi utapata kujua mengi kutoka kwake.
Designed By Nyang'aya Zakayo ( a.k.a Dazzy ) |
Kwa hali hiyo basi kijana aliona ni vema kuweza kutushirika katika kupata elimu juu ya mazingira ambayo ameyapitia maana ana uwelewa wa kutosha juu ya maisha haya hapa utapata kujua zaidi Jinsi maisha yenyewe yalivyo uzuri wake na ubaya wake, Mazingira yenyewe utapata nafasi ya kuona picha za mazingira hayo.
Wakazi wanapata changamoto gani katika mazingira yao, shughuli zinazofanyika katiaka mazingira hayo, na utapata mengine mengi amabayo hata wewe itakuwa ni mara ya kwanza kuyasikia hapa. Unakaribishwa sana katika kupata habari hiz pindi hii website itakapokuwa imekamilika na kuwekwa hewani.
Designed By VICTOR MANDARA ( King Mandara Jonior ) |
Hii ni Muundo au mwonekano wa website hii itakavyokaa kwa lugha ya kigeni tunaiita ( TEMPLATE ). Hapa kijana huyu amejipanga kutuelezea zaidi kuhusu Biashara hii ambayo inafanywa na akina mama mtaani kwake. Kulingana na elimu ya web design aliyoipata Musoma Information Center. Na walipofikia kwenye hiki kipindi cha kutuelezea kwa kutumia tovuti ( website ) vile vitu vinafanyika mtaani kwao ambavyo vinaweza kutuvutia na sisi kuweza kutembelea website yake na kuweza kusoma na kuvielewa kijana kaja na " WOMEN TRADE " akimaanisha biashara za akina mama mtaani. Hapa tutapata kujua mengi kuhusiana na biashara hizi zikiwemo faida wanazozipata, hasara wanazozipata, changamoto wanazozipitia, Jinsi gani tunaweza wasaidia kwa wale wenye moyo wa kusaidia, na vingine vingi ni hapahapa usibanduke.
|
0 comments:
Post a Comment